AUDIO SINGELI

DJ MUSHIZO ASHUSHA NDINGA MBILI

Msanii, producer na DJ maarufu, DJ Mushizo, amethibitisha kununua gari mbili mpya aina ya Alphard na Crown. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, DJ Mushizo alishare picha za magari hayo na kuandika:

RELATED : AUDIO | Meja Kunta Ft. Ibraah x Jay Combat – Kwani We Nani Remix | Download

“ASANTE MUNGU Kwa Kuniwezesha Kutimiza Moja ya Malengo yangu Ya Kuweza Kupata GARI 2 CROWN, ALPHARD. Hakika Haikuwa Rahisi Kabisa Hii ni Ndoto ya Zaidi Ya Miaka 5 Nyuma Hakika hii ni kubwa sana Kwangu. Na Pia Nitoe Shukran kwa Mashabiki zangu wote mnaonisapoti Nawapenda sana na Muendelee kunisapoti Zaidi Asanteni” – DJ Mushizo.

Huu ni ushuhuda wa juhudi, bidii na kujitolea kwa DJ Mushizo ambaye amekuwa akifanya kazi kwa miaka mingi kufikia mafanikio haya. Hongera kwa mafanikio haya makubwa!

Kwa habari na matukio ya wasanii mbali mbali, usiache kutufollow IK Mziki.

#DJMushizo #Alphard #Crown #MusicNews #IKMziki