Tunasikitika kutangaza kifo cha msanii wa filamu Hawa Hussein Ibrahim, maarufu kama Carina au Caren, kilichotokea leo Aprili 15, 2025, nchini India.
Carina alikuwa nchini humo kwa matibabu ya tatizo la tumbo ambalo lilimsumbua kwa miaka mingi. Alifanyiwa upasuaji mkubwa na alitarajiwa kurejea Tanzania leo.
Kifo chake kimethibitishwa na rafiki yake wa karibu, Imelda Mtema.
Alisafiri kwenda India Februari 24, 2025 baada ya michango mbalimbali kukamilisha gharama za matibabu kiasi cha Sh54 milioni.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi zitatolewa baadaye.
Tutaendelea kukuenzi milele.
#RIPCarina #ikmziki #Tanzania